Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini DPP, leo Machi 4, 2022 Amemfutia mashtaka yote ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu kwa sababu hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Hata hivyo, washtakiwa hao hawakufikishwa mahakamani kwa sababu Mshtakiwa wa 4 Freeman Mbowe ni mgonjwa kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Magereza.
DPP ameondoa mashtaka hayo mbele ya Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ambapo Washtakiwa hao leo walipaswa kuanza kujitetea.