Mfano wa Tuzo
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza majina ya wasanii walioteuliwa kuwania tuzo za muziki ambapo wasanii kutoka lebo ya wasafi hawapo.
Orodha hiyo imetolewa leo Jumamosi Machi 19, 2022 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko na katika orodha hiyo haina msanii hata mmoja kutoka lebo ya Wasafi huku sababu ikielezwa kuwa hawakupeleka kazi zao wakati wa kukusanya ambapo wasanii 1360 ndio waliopeleka. TAZAMA ORODHA CHINI
Hata hivyo mnamo Machi 14, 2022 katika kipindi cha the switch cha wasafi Fm wakati CEO wa WCB wasafi Nasib Abdul Maarufu Diamond Platnumz akihojiwa alisema kuwa suala la tuzo za muziki Tanzania ni zuri ila hayuko tayari kushiriki.
Alisema kuwa sababu ni kuwa anataka kushiriki tuzo za kimataifa ili alete heshima nchini huku akidai kuwa kama WCB ikishiriki tuzo zote wanaweza kuchukua wao.
TAZAMA HAPA CHINI WASANII WALIOCHAGULIWA KATIKA VIPENGELE VYA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA