Breaking

Wednesday, 23 March 2022

BASATA YAINGILIA KATI SAKATA LA UTEUZI WA STEVE NYERERE KUWA MSEMAJI WA SMT



Wakati kukiwa na mgawanyiko miongoni mwa wasanii wa muziki kuhusu uteuzi wa Steve Nyerere kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), Baraza la Sanaa la Taifa(Basata), limesema pande zote mbili zina hoja na hivi karibuni watalitolea majibu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Machi 23,2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko,muda mfupi baada ya kumaliza kikao na viongozi hao kilichoketi takribani saa tano.

Mniko amesema kuwa waliziita pande zote mbili za uongozi na wakawasikiliza na kugundua kila upande una hoja na Basata watatoa uamuzi wa jambo hilo hivi karibuni.

"Moja ya majukumu tuliyopewa Basata ni kushughulikia pia migogoro inapotokea kwa wasanii nasi tulichofanya leo ni moja ya jukumu hilo kwa kuwaita na kuwasikiliza kila upande na hoja zao" Amesema

Amesema kuwa baada ya kumaliza kupitia hoja zao baraza hilo litatoa majibu mapema iwezekanavyo katika kumaliza mgogoro huo.

"lengo sio kuona wasanii wanafarakana bali tunataka wafanye kazi kwa kushirikiana na kuipeleka sanaa mbele," amesisitiza Katibu huyo.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages