Breaking

Friday, 4 March 2022

AMCHINJA MKEWE NA KISHA AJINYONGA



Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nsekwa wilaya ya Mlele mkoani Katavi anayejulikana kwa jina la Anisent John mwenye umri wa miaka 32 amemchinja mkewe kwa panga sehemu ya shingoni kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia chandarua.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi ACP Ally Makame,  amesema mtuhumiwa ambae ni marehemu alifunga mlango wa chumba chao kisha kumuua mkewe na yeye kujinyonga kwa kutumia chandarua alichokifunga juu ya kenchi.

Kamanda Makame amesema kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi la polisi kwa sababu tukio hilo limetokana na mgogoro wa kifamilia na mtuhumiwa wa mauaji hayo naye amekufa kwa kujinyonga.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages