Mwili wa mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Mzuzu umeokotwa katika mtaro wa maji mtaa wa Kazima kata Isevya manispaa ya Tabora.
Mwenyekiti wa mtaa huo Amani Mohamed amesema mwili wa marehemu ulikua na majeraha na kidole kimoja cha mguu wa kushoto kimekatwa mpaka kimening'inia na pembeni ya mwili wake kumekutwa fimbo zenye damu na kwamba kuna dalili kuwa mwanaume huyo ameuwawa na watu wasiojulikana.
Kwa upande Mayasa Adam jirani na eneo tukio lilipotokea amesema usiku wa kuamkia 28 March majira ya saa 5 kulikua na kelele za mwanaume akiomba msaada.
"Uwiii na kufaaa nisaidieni naombeni basi hata maji ya kunywa" alisikika akiomba msaada marehemu.
Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi!
Source: cgfmradio