Watu saba wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa kutika ajali iliyohusisha lori aina ya Scania kugonga Bajaji katika barabara ya Bariadi - Maswa mkoani Simiyu.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu, ACP Blasius Chatanda ameeleza kuwa jana Jumapili Machi 27, 2022 majira ya saa moja na nusu usiku lori aina ya Scania lenye namba za usajili T172 AUP, liligongana na Bajaj yenye namba za usajili MC 426 CFQ katika eneo la Kidulya wilayani Bariadi.
Kamanda Chatanda amewataja watu waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Joseph Nsungi Sasa (31) Mkazi wa Bunamala, Lameck Sayi Lyaganda, (32) mkazi wa ibulyu, Pagi Hima Peme, (16)mkazi wa Ibulyu, Joseph Nzumbi (22) mkazi wa Kidalimanda, Shinda Maige Hima, (17) mkazi wa Ibulyu, Susa Sayi (18) mkazi wa Ibulyu na Masunga Dotto Mbilibili, (32) ambaye ni dereva wa Bajaji.
Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti na Majeruhi Wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Mji ya Bariadi.
Aidha ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi uliosababisha dereva wa lori hilo kushindwa kulimudu na kugonga Bajaji ambayo iliungua Moto baada ya ajali.
Ameongeza kuwa derava wa roli alikimbilia kusikojulikana, na jitihada za kumtafuta zinaendelea.
SOMA: SALMA HIJAB FASHION..! JIPATIE MITANDIO | HIJAB NA ABAYA KWA BEI NAFUU