Watu 22 wamefariki huku 38 wakijeruhiwa katika ajari iliotoke eneo la melela kibaoni barabara ya iringa-morogoro baada ya basi la kampuni ya Ahmed likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana na Lori la lilikokuwa likisafiri kwenda nje ya nchi.
Ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Machi 18, 2022 majira ya saa 11 jioni, eneo la Melea Kibaoni, njia panda ya Kilosa katika barabara kuu ya Morogoro - Iringa na kusababisa vifo vya wanaume 15, wanawake 6 na mtoto mmoja wa kiume.
Akithibisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu amesema kuwa basi lenye namba T 732 ATH aina ya Scania kampuni ya Ahmed lilikuwa safarini kutokea Mbeya kwenda Tanga liligongana na Roli aina ya Howo lenye namba IT 2816.
Amesema kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa Dereva wa Roli kutokana na kutaka kuipita pikipiki (overtake) bila kuchukua tahadhari kabla ya kugongana na basi hilo.