Breaking

Sunday, 20 February 2022

WAZIRI MKUU AONGEZA SIKU SABA UCHUNGUZI MAUAJI MTWARA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongeza siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Februari 20, 2022 na ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022.

Taarifa imeeleza kuwa kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.

Kamati hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa Februari 4, 2022 mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Aidha Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi.

Hivi karibuni askari saba wa Jeshi la Polisi walipandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya mfanyaniashara wa madini  mkoani Mtwara huku wa nane aliyekabiliwa na tuhuma hizo akijinyonga alipokuwa mahabusu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages