Breaking

Tuesday, 22 February 2022

WATU 60 WAFARIKI KATIKA MLIPUKO WA MGODI - BURKINA FASO



Takriban watu 60 wamefariki dunia baada ya mlipuko kutokea katika mgodi wa dhahabu Gaoua kusini-magharibi mwa Burkina Faso.

Mlipuko huo umetokea jana Jumatatu Februari 21,2022 katika ghala la mada za kemikali zinazotumiwa kusafishia madini ya dhahabu.

Makumi ya watu zaidi walijeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto ambao walipelekwa katika hospitali ya mkoa ya Gaoua.

Sansan Kambou ambaye ni mlinzi wa mazingira aliyekuwepo eneo la tukio hilo amesema maiti nyingi za watu zilitapakaa huku na kule.

Burkina Faso ina kasi kubwa ya uzalishaji wa madini ya dhahabu barani Afrika na kwa sasa inashika nafasi ya tano katika uzalisha wa madini hayo.

Karibu watu milioni 1.5 wanafanya kazi katika sekta ya madini ya dhahabu nchini Burkina Faso na thamani na uzalishaji wa tasnia hiyo mwaka 2019 ilitangazwa kuwa ni karibu dola bilioni 2. 

Ajali hutokea mara kwa mara katika shughuli za uchimbaji madini ambazo hazijaidhinishwa katika baadhi ya nchi za Afrika, huku udhibiti wa usalama mara nyingi ukiwa mdogo au haupo kabisa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages