Na OR-TAMISEMI
Waziri Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Februari 23, 2022 katika kikao cha Baraza la Madiwani wilayani Karagwe kilichofanyika ukumbi wa Agaza, Karagwe, mkoani Kagera.
“Mheshimiwa Rais kwa kutambua kazi nzuri wanayofanya watendaji wa kata kote nchini aliamua kuwawezesha kwa kutoa posho ya madaraka, hiyo posho sio kwa hisani ipo kisheria, naelekeza halmashauri zote nchini kuhakikisha kila mwisho wa mwezi wanatoa posho ya madaraka kwa wakati na ziwakute walipo,” amesema Waziri Bashungwa.
Aidha, Waziri Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya Karagwe, Julieth Binyura kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kuhakikisha anasimamia na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imekithiri katika Wilaya hiyo na kusababisha umasikini kwa wananchi.
Akizungumzia upungufu wa walimu wa sayansi nchini, Waziri Bashungwa amesema ili kupunguza uhaba huo kwenye kibali cha ajira za walimu kitakachotolewa na Rais, walimu wa sayansi watapewa kipaumbele na mpango huo utaenda sambamba na ujenzi wa mahabara katika shule za sekondari na matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari
Waziri Bashungwa ameeleza kuwa malengo ya Wilaya ya Karagwe ni kuwa na Shule tatu za kidato cha tano na sita hivyo ifikapo Aprili mwaka huu Serikali itatoa fedha kukamilisha shule za sekondari za Kituntu na Nyabiyonza.