WAKALA wa Barabara za Vjjijini na Mijini (TARURA) kwa kusirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya wamefanikiwa kukamata magari matatu yaliyokuwa yakitoroshwa na Mkandarasi ambaye ni Milembe Construction Company Ltd katika Kata ya Chimala Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Hayo yamejiri baada ya TARURA kuvunja Mkataba uliokuwa unatekelezwa na Mkandarasi huyo wa ujenzi wa Barabara ya Inyara – Simambwe kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 16.7 na kuelekeza kuwa vifaa vyote vya Mkandarasi viendelee kubaki eneo la kazi hadi mradi huo utakapokuwa umekemilika na hii ni kwa mujibu wa Mkataba.
Akiongea katika mahojiano maalum, Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Wilson Charles ameeleza kuwa wamepata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa magari matatu yametoroshwa hivyo ilibidi kuwasiliana na Jeshi la Polisi na wakafanikiwa kuyakamata magari hayo.
’’Sheria inatuelekeza baada ya kuvunja Mkataba kushikilia vifaa vyote vya Mkandarasi hadi hapo mradi utakapo kamilika,kitendo hiki cha kutorosha vifaa hakikubaliki na ni kinyume na Mkataba,"amesema Mhandisi Wilson.
Ujenzi wa Barabara ya Inyara – Simambwe kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita Mkandarasi huyo alitekeleza mradi kwa kusuasua suala lililopelekea TARURA kuvunja Mkataba huo ili apatiwe mwingine atakayeweza kukamilisha kwa wakati.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990