Watu wawili wakazi wa Kijiji cha Ololosokwani wilaya ya Ngorongoro wamejeruhiwa kwa kupigwa na radi baada ya kutumia simu wakati mvua ikinyesha.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi MKoa wa Arusha kamishina msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa Mnamo Februari 17,2022 SASINES ONAROK maarufu kama BABU (25) mkazi wa ololosokwani na mwingine ni KISHUYAN TERYA maarufu kama KIYOMI(28) walijeruhiwa na radi wakati wakiwa machungani ambapo mvua ilikuwa ikinyesha.Kamanda Masejo ameeleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni matumizi ya simu wakati mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kuambatana na radi ambayo ilipelekea wahanga hao kujeruhiwa sehemu mbalimbali ya mili yao na radi hiyo.
majeruhi hao walikimbizwa katika zahanati ya kijiji cha ololosokwani na kupatiwa matibabu.
Aidha Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari hasa kipindi cha mvua kubwa ambazo huambatana na radi kali,Pia amewataka kuacha mara moja matumizi ya vifaa vya umeme ikiwemo simu wakati wa mvua kwani kwa kufanya hivyo kuta waepusha na madhara makubwa ya nayoweza kutokea.

Mwisho