NA MWANDISHI - WMNN
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameliagiza Jeshi la Polisi kuwawajibisha askari watakaokiuka maadili kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutendaji.Naibu Waziri Sagini alizungumza hayo Jumatatu Februari 21, 2022, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam, wakati alipokutana na Sekretarieti ya Usalama Barabarni kwa lengo la kujitambulisha kwa wajumbe wa Sekretarieti hiyo pamoja na kufahamu utendaji kazi wao.
“Nimefadhaishwa na askari wanaokiuka maadili ya kazi. Wale wanaokiuka maadili wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu ili Jeshi letu la Polisi liendelee kuaminiwa na kuheshimika,” amesema.
Aidha, Naibu Waziri Sagini ameipongeza Sekretarieti ya Usalama Barabarani kwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara kwa wananchi na kupunguza ajali zinazopelekea vifo, majeruhi na uharibifu wa miundombinu.
“Niwahimize, maagizo mnayopewa na Viongozi wenu na yale ambayo tumeagizwa na Mheshimiwa Rais tuhakikishe tunayafanyia kazi haraka,”amesema.

“Ninawapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yenu ya kuhakikisha kuna kuwepo hali ya usalama barabarani hasa kwa kutoa elimu kwa Watanzania nakupelekea kudhibiti ajali nchini,”amesema.
Akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya Usalama Barabarani, amewataka kuharakisha utekelezaji wa maelekezo waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ya ununuzi wa vitendea kazi kwa kuyapa kipaumbele katika mpango kazi wao.
“Niwahimize, maagizo mnayopewa na Viongozi wenu na yale ambayo tumeagizwa na Mheshimiwa Rais tuhakikishe tunayafanyia kazi haraka,”amesema.