Mwanamke mmoja anayeitwa Joan Burke mwenye umri wa miaka 61 mkazi wa jimbo la Florida nchini Marekani, amekamatwa kwa tuhuma za mauaji baada ya kudaiwa kumchoma na kisu mume wake kwa zaidi ya mara 140 na kupelekea kifo chake.
Kulingana na ripoti ya polisi ya kituo cha Palm Springs imesema kuwa siku ya Ijumaa Februari 11,2022walipigiwa simu na Ricardo Green (41) aliyedai kuwa ni mtoto wa mtuhumiwa alipiga simu 911 jioni ya kusema kwamba alirudi nyumbani kutoka kazini na kumkuta babake wa kambo, Melvin Weller (62) amelala sakafuni kwenye dimbwi la damu akionekana kuwa amekufa.
Polisi walifika eneo la tukio na kukuta mwili wa Melvinukiwa amezunguukwa na dimbwi la damu sakafuni.
Baada ya kufanya uchunguzi walikuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha mengi, pamoja na madoa ya damu yaliyotolewa au kuenea kwenye kuta, dari, kaunta na makabati ikionesha kuwa alishambuliwa na kitu chenye ncha kali.
Uchunguzi wa daktari ulionyesha kuwa marehemu alipata majeraha zaidi ya 140 ya kuchomwa kisu mwilini mwake na alipasuka fuvu kwa kupigwa na kisu cha nyama.
Polisi walimkamata Joan Burke ambaye ni mke wa marehemu akiwa chumbani kwake ambapo hakutaka kuzungumza chochote.
Burke alionekana kuwa na majeraha kwenye viganja vya mikono yote miwili ambapo polisi wamesema kuwa ni jambo la kawaida kwa mhalifu kupata majeraha kwenye kiganja cha mkono mmoja au wote anapomdunga mtu mwingine.
Kuchomwa kwa visu mara kwa mara husababisha damu kuingia kwenye mpini wa kisu na kwenye mikono ya kisu, na kusababisha mshiko wa kisu kuteleza na kupasua ngozi yao kwa ubao.
Hakimu wa Kaunti ya Palm Beach aliamuru Burke awekwe kifungoni bila dhamana.